MENDE ni moja ya kichocheo cha Pumu na Mzio (Aleji)


Mende si kero tu ndani ya nyumba; wanaweza pia kuathiri afya yako. Kinyesi, mate na mabaki ya miili yao vina protini zinazoweza kusababisha mwitikio wa mzio (aleji) kwa baadhi ya watu.

Unapovuta hewa yenye chembechembe hizo, unaweza kupata dalili kama kupiga chafya, mafua, kuwashwa macho na ngozi. Kwa watu wenye pumu, vichocheo hivyo vinaweza kuzidisha kukohoa, kubanwa kifua na kupumua kwa shida.

Jilinde kwa kuweka mazingira safi, kufunika vyakula, kutupa taka kwa wakati na kudhibiti mende nyumbani.