Mtu anaweza kuwa na Kaswende kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili zozote.


Hali hii hujulikana kitaalamu kama Kaswende isiyoonyesha dalili (Latent Syphilis). Katika hatua hii, bakteria wanaosababisha kaswende (Treponema pallidum) wanakua bado wapo mwilini na maambukizi yanaendelea kuwepo, lakini mtu haonyeshi dalili zinazoonekana.

Wakati huu, mfumo wa kinga ya mwili unaendelea kukabiliana na maambukizi, lakini hauwezi kuhakikisha kuwa bakteria wote wameondolewa. Hivyo, mtu anaweza kujisikia mzima kabisa huku maambukizi yakiendelea kuwepo mwilini. Hatua hii inaweza kudumu kwa miaka kadhaa bila mtu kutambua kuwa ana kaswende.

Kutokuwepo kwa dalili hakumaanishi kuwa ugonjwa umeisha. Bila matibabu, kaswende inaweza kuendelea na baadaye kusababisha madhara makubwa kwenye moyo, ubongo, mishipa ya fahamu na viungo vingine vya mwili.

Kaswende inatibika kwa antibiotiki. Uchunguzi na matibabu ni muhimu hata kama mtu hana dalili.

Usisubiri dalili ndipo upime. Ikiwa umekuwa katika hatari ya kupata maambukizi au mwenza wako amegundulika kuwa na kaswende, nenda kituo cha afya kwa uchunguzi.