Je, unajua kwa TSh 150,000 kwa mwaka, unaweza kupata kifurushi cha bima ya afya kinachojumuisha watu hadi sita!
Kifurushi hiki kinajumuisha:
Mwanachama mkuu, wewe.
Mume au mke.
Wategemezi wengine wasiozidi wanne, ambao wanaweza kuwa:
Mama au baba yako.
Mama au baba wa mwenzi wako.
Watoto wako wa kuzaa, wa kuasili (adoption) au wa kambo walio chini ya miaka 21.
Ndugu zako wa damu, kama kaka au dada, walio chini ya miaka 21.
Hii ina maana kwamba unaweza kumjumuisha hata mzazi wako au mtoto wa kambo, mradi wategemezi wote wanakidhi masharti ya skimu.
Je, ungependa kujua huduma za afya zinazopatikana kupitia kifurushi hiki? Endelea kufuatilia Bonge la Afya.
