Anayekunywa pombe, hata vinywaji vikali, bado anaweza kupata minyoo


Kuna watu wanaoamini kuwa kunywa pombe kali kama Konyagi kunaweza kuua minyoo tumboni, huu ni mtazamo usio sahihi kisayansi.

Pombe haifanyi kazi kama dawa ya minyoo. Unapokunywa Konyagi au kinywaji kingine chenye kilevi, pombe huingia kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kufyonzwa mwilini. Haifiki kwenye utumbo kwa kiwango kinachoweza kuua minyoo.

Kwa hiyo, hata mtu anayekunywa pombe kali anaweza kuwa na minyoo. Kunywa pombe nyingi kwa lengo la kutibu minyoo hakutasaidia, na kunaweza kuathiri afya ya ini na viungo vingine.

Minyoo hutibiwa kwa dawa maalumu zinazochaguliwa kulingana na aina ya maambukizi. Ikiwa unahisi una minyoo, pata ushauri wa mtaalamu wa afya badala ya kutumia pombe kama tiba.