Nigeria Yathibitisha Kesi ya Kwanza ya Ebola: Mgonjwa Alitoka Uganda, Watu 44 Wafuatiliwa

 

Nigeria imethibitisha kisa cha ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo, baada ya mwanamke mmoja kupatikana na maambukizi jijini Abuja, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 20 Oktoba 2026 na Dkt. Muhammad Ali Pate, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Nigeria, vipimo vya maabara vilithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa ameambukizwa virusi vya Ebola. Shirika la Afya Duniani (WHO) pia lilithibitisha taarifa hiyo siku hiyo.

Mgonjwa alitoka wapi, na nini kilitokea?

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, mwanamke huyo alikuwa na historia ya hivi karibuni kusafiri kwenda kwenda Uganda na aliwasili Nigeria siku nne kabla ya dalili kuanza.

• 7 Oktoba 2026: Mwanamke huyo alianza kuonyesha dalili za ugonjwa.

• 11 Oktoba 2026: Alikwenda kupata huduma katika hospitali binafsi jijini Abuja.

• 20 Oktoba 2026: Kipimo cha maabara kilithibitisha maambukizi ya virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo.

Baada ya kuthibitishwa kwa maambukizi, mwanamke huyo aliwekwa kwenye eneo maalumu la kutengwa na anaendelea kupata huduma za matibabu.

Ingawa mwanamke huyo alikuwa na historia ya safari inayohusisha Uganda, mamlaka zinaendelea kuchunguza mahali alipoweza kuambukizwa. Kufikia tarehe 20 Oktoba, mamlaka za afya nchini Nigeria zilikuwa zimetambua watu 44 walioweza kuwa wamekutana na mgonjwa huyo. Watu hawa wanafuatiliwa ili kubaini kama wataonyesha dalili na kuchukua hatua zinazofaa mapema.